
“Kwa jina la Mwenyezi Mangu (Alla) mwenye rehema, mtawala wa ulimwengu, Mwenye rehema, mwenye huruma. Sifa ziwe kwa mungu mtawala wa mbingu, mwenye rehema, mwenye huruma wa siku ya Kiyama.
Wewe tu tunakuabudu, na wewe peke yako tunakuomba msaada. Tuongoze katika njia adilifu, njia za wale uliowabariki,
siyo wale wanaostahili ghadhabu
wala za wale waliopotea.”
Waislamu ni sharti wakariri sura hii kabla ya kufanya kazi zo zote za siku. Katika kaligrafia za kiarabu beti hii inaweza kuanzwa kwa jinsi na mpango usiohesabika.
Mfumo wa Sheria
Usultani umeweka sahihi kwa sheria kulingana na sheria ya dola ya mataifa (UN) hasa zile zinazohusika na ulindaji wa haki za binadamu, kulindwa kwa wachache (minority) vilevile makubaliano dhidi ya aina yo yoto ile ya ubaguzi wa wanawake ha haki za mtoto.
Utawala wa sheria, mamlaka ya taifa, uhuru wa mahakama ni mojawapo za kanuni zilizowekwa ili kulinda haki za kila mwananchi wa Omani. Kila mshtakiwa anakisiwa kuwa bila hatia mpaka ithibitishwe kwamba ana hatia kupitia daawa. Utumiaji wa matusi ya kimwili au kisaikologia umekatazwa. Adhabu zo zote zile ni lazima zifuatane na sheria kwani wananchi wote ni sawa mbele ya sheria.