Mastadi juu ya Uibadhiyah

Falsafa ya Uibadhiyah inavutia sana sana usikivu wa mashirika ya utafiti ya kilimwengu. Baadhi ya watalaam muhimu wanaofanya kazi katika eneo hili watatambulishwa katika ukurasa huu.

John C. Wilkinson

John C. Wilkinson, D. Litt, ni profesa mshiriki wa awali katika chuo kikuu cha Oxford na ni profesa wa heshima mstaafu wa chuo cha St. Hugh, Oxford ambapo alifunza kuanzia mwaka wa 1969 hadi 1997 alipostaafu.

Alifanya kazi kwa miaka mingi na makampuni ya mafuta huko Mashariki ya Kati kabla ya kurudi Oxford kuandika tasnifu yake juu ya Uibadhiyah wa Usultani wa Omani.

Yeye ni mwandishi wa makala mengi na vitabu kadhaa hasa: Maji na Ukaazi wa makabila katika Kusini-mwa Uarabunik Mashariki (Clarendon Press, 1977), Mila za Uimanu wa Omani (Cambridge University Press, 1987), Mipaka ya Uarabuni (I. B. Tauris, 1991) na Uibadisim: Asili na maeondeleo ya mapema katika Omani (Oxford University Press, 2010).

Valerie Hoffman

Valerie Hoffman ni mkurugenzi wa kituo cha masomo ya Asia Kusini na mafunzo ya Mashariki ya Kati katika Chuo Kibuu cha Illinois.

Yeye ni mtaalam wa falsafa ya Uislamu na mazoea na amafanya kazi juu ya vipengele vingi kuhusu Uislamu, kuanzia wakati wa Mtume mpaka leo hii; amefanya uchunguzi wa maandishi na kazi ya utafiti wa uwandani. Muhula wa mafunzo wa mwaka 2000 - 2001 alikaa Omani na Hadramawt, na alivutiwa sana na falsafa ya Uibadhi ya Uislamu.

Angeliki Ziaka

Dk. Angeliki Ziaka ni mhadhiri wa Hisoria ya Dini katika Chuo Kikuu cha Aristotle Thessaloniki, na Daktari (filisofia) katika Chuo Kikuu cha Marc Bloch Strasbourg.

Yeye anabobea mafunzo ya usanifu ya Uislamu na Ustaarabu wa kiarabu/kiislamu na katika mada kuhusu mazungumzo na mwingiliano wa kidini ambao ameufanyia utafitik kwa undani katika Chuo Kikuu cha Strasbourg, pia katika Taasisi ya Uchunguzi wa mafunzo ya Kiarabu na Kiislamu (PISAI, Roma), pia Chuo Kikuu cha Amman (Jordan). Utafiti waka unalenga hasa juu ya theolojia za Usilamu na hisoria vilevile, kadiri za kijamii, kidini, kisiasa za Uislamu katika Mashariki ya Kati.

Amehariri kitabu juu ya Ibadism ambacho kinaonyesha mambo yanayoendelea ya mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu Uibadhism na Usultani wa Omani,uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Aristotle Thessaloniki Novemba 2009.

Heinz Gaube

Heinz Gaube ni profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Tuebingen Ujerumani ambapo alifunza Masomo ya Kiirani. Baada ya kustaafu alizingatia uendelezaji wa Uibadhism katika eneo la Bahari Hindi.

Katika kitabu chake, Ibadis katika eneo la Bahari Hindi anaonyesha kwa mara ya kwanza ukaguzi wa undani wa ushaidi wa ki akiolojia wa wakati wa Kiislamu katika pwani ya Kenya na Tanzania, vilevile vianzo vya maandishi yanayohusikana na Afrika, ya mashariki na lugha za Ulaya na inatoa usanisi juu ya asili mbalimbali ya vianzo.

Ersilia Francesca

Ersilia Francesca ni profesa mshiriki wa Hisoria ya Dunia ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha "L'Orientale" cha Naples. Kuanzia mwanka wa 2005, yeye amekuwa mwanachana wa Shirika la Kimataifa la Masomo ya Sheria za Uislamu (ISILS – Chuo Kiuu cha Harvard).

Kati ya uchapishaji wake ni: Nadharia na utekelezaji wa biashara wakati wa Enzi ya Kati katika Uislamu. Mikataba ya kuuza na sifa kuliangana na haki za Uibadi, Rome 2002.

Mnamo mwaka wa 2014 kitabu Thelojia ya Ibadi. Nyanzo za marejeo na kazi za kitaalam, ambacho alikihariri, kitachapishwa. Lengo la nakala hii ni kutafiti hoja tofauti za theolojia ya Uibadhi kuanzia mwanzoni hadi sasa.

Wataalamu wengi wengineo:

Agostino, Cilardo
Chuo Kikuu cha "L'Orientale" cha Naples
http://docenti.unior.it/index2.php?user_id=acilardo&content_id_start=1




Aillet, Cyrille
Profesa msaidizi, Historia ya Uislamu Enzi ya Kati, Chuo Kikuu cha Lyon, Ufaransa
http://univ-lyon2.academia.edu/CyrilleAillet

Badry, Roswitha 
Semina ya utaalamu wa mambo ya nchi za Mashariki, Chuo Kikuu cha Albert-Ludwigs-Universität Freiburg, 
Ujerumani
https://www.orient.uni-freiburg.de/islam/mitarbeiter/badry

Chiarelli, Leonard
Maktaba ya J. Willard Marriott katika Chuo Kikuu cha Utah
http://campusguides.lib.utah.edu/middleeast

Gaiser, Adam
Profesa Mshiriki wa dini, Chuo Kikuu cha Florida, USA
religion.fsu.edu/faculty_adam_gaiser.html

Madelung, Wilferd
Chuo Kikuu cha Oxford. Kwa sasa yeye ni mtifiti mkubwa katika Taasisi ya Masomo ya Ismaili mjini London
http://www.iis.ac.uk/view_person.asp?ID=54&type=auth

Radivilov, Danylo
Naibu wa Mkurungenzi Taasisi ya Utaalamu wa mambo ya Nchi za Mashariaki, Kiev, Ukraine
http://www.islamicmanuscript.org/DirectoryOfMembers/Person.aspx?mid=134

Rohe, Mathias
Chuo Kikuu cha Erlangen-Nuremberg, Ujerumani
http://www.religareproject.eu/content/mathia

van Ess, Josef
Chuo Kikuu cha Tuebingen, Ujerumani
http://de.wikipedia.org/wiki/Josef_van_Ess