Hulka za wanawake katika Omani
Wanawake wanashikilia vyeo katika wizara katika Usultani na wameshateuliwa kuwa mabolozi nchi za ng’ambo. Wabunge wanawake wapo katika Majlis A’Shura (Baraza la uelekezi) pia Majlis A’Dawla (Baraza la Taifa). Wanawake wanashikilia vyeo rasmi katika daraja zote, wanatoa huduma katika jeshi na nusu ya wafanyakazi wa serikali ni wanawake.
Katika sekta binafsi utakuta wanawake wakifanya kazi sio tu za kawaida bali katika vyeo vya uongozi (menejimenti), vyeo vya utendaji vilevile kama katibu mkuu mtendaji yaani (CEO) pia wao ni wamiliki mali. Hakuna tasnia yo yote iliyofungiwa wanawake. Sheria ya Omani inadhamini likizo ya malipo ya uzazi, pia malipo sawa kwa kazi sawa.
Sheria zote zilizopo kwa sasa na kanuni katika Omani hutao nafasi sawa kwa wanawake katika kufanya biashara, huduma za kiserikali na bima za kijamii.
Serikal ilianzisha vituo vya kujifunza kusoma na kuandika na ilifanya swala kuhusu elimu kuwa la lazima kwa wasichana, jambo lenye mafanikio. Tangu hapo asilimia ya wanawake wanaosoma imeongezeka mpaka kwamba imekuwa muhinu kuweka idada ya kikomo kwa wanaume katika Chuo Kikuu Cha Sultani Qaboos.
Vilevile kuna vyama na mashirika mbalimbali ambayo yanahusika na maswala ya wanawake. Hawa wamekabidhiwa wajiba wa kusomesha, kufanza na kufafanua zaidi uwezekano kwa wanawake. Hata kama mwanamke ameolewa au hajaolewa, ni lazima awe na fursa ya kupata mapato yake na hii inanchagia hali ya kujimudu kiuchumi katika familia.
Katika misikiti mingi mtu atakuta vyumba vya sala maalum vya wanawake tu. Hapa wanawake wanajifunza juu ya dini na Quran kutoka kwa wanawanke wengine waliopata ujuzi maalum katika maswala haya. Kutimiza lengo hili “kituo cha mafunzo ya dini cha wanawake” kilianzishwa, mahali ambapo wanawake wanafunza pia.