Misikiti katika Omani iliyojengwa kiasili
Misikiti ambayo ilijengwa kwa utamaduni wa Ibadhi ilikuwa ya miundo ya kawaida na haina minara (ya misikiti). Kuta za ndani ya misikiti zilikuwa za kawaida lakini mara kwa mara zilipambwa kwa nakshi na kaligrafia katika kishuba cha sala, pia juu kwenye dari za mbao.
Kabla ya kitendo cha sala huwa ni muhimu kujitakasa, kwa hivyo kwa kawaida misikiti ilijengwa mahali penye chemicheni za maji, karibu na visima au mifereji yaani aflaj. Wakati huu wa utoaji wa maji kupitia manispaa, misikiti hujengwa po pote pale, mara nyingi na vyumba mbalimbali vya sala, vya wanaume na wanawake.