Uibadhiya

Uibadhiya ni falsafa tofauti kuhusu Uislamu, hata Suni wala Shia, ambazo ziliibuka nyakati zu mwanzoni za Uislamu (Uibadhiya) umebaki katika mifuko ya wachache huko Afrika na ni yenye nguvu huko Omani.

"Uislamu wa Ibadhi umechukuwa jukumu muhimu katika historia na mawazo ya kiislamu na unaenadelea kuwa na nguvu katika maisha ya kisasa ya nchi za Mashariki ya Kati na Afrika".

Brannon Wheller, mwandishi wa kitabu "Maka na Edeni: Matambiko, Kumbukumbu, na Maeneo ya Uislamu", katika tafakari yake ya kitabu cha Valerie Hoffman kiitwacho "Mambo muhimu ya msingi katika Uislamu wa Ibadi".



Ibadhis ilianzishwa na Abd Allah ibn-Ibad huko Basra katika miaka ya 680s kama kundi la kadri lililopinga uasi wa kutumia silaha na mauaji ya kisiasa na walikuwa radhi kuishi na Waislamu wangineo.

Katika theolojia Ibadhis hukataa tafsiri halisi ya rahisi ya maelezo ya mungu kufanana na binadamu, Ibadhi hunyima watu fikra za uwezekano wa kumwona Mungu maishani au baada ya kifo (ahera).

Pia kuna Waibadhis katika nchi nyingine kwa mfano Libya, Tunisia, Algeria, nchi za Afrika Mashariki hata Uchina.