Kituo cha Al-Amana mjini Muscat katika Usultani wa Omani

Kituo cha Al Amana hufanya kazi kimataifa kwa ajili ya mema ya kawaida kwa kujenga madaraja ya uelewano na ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo.

Mnamo mwaka wa 1893 kanisa la Kiprotestanti la Amerika liliwasili Omani na kuanza kazi ya tiba na elmu. Hii ilifanikiwa tu kwa sababu ilikuwa ni juhudi za pamoja na wananchi na wakaazi wa Omani wenye madhehebu mbalimbali ambao walifanya kazi bega kwa bega ili kutumikia maslahi ya jamii nzima.

Pamoja na maendeleo ya kisasa ya nchi, kazi hii ilifikia mwisho, lakini maono mapya yaliibuka kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hii. Kituo cha Al Amana kilianzishwa mnamo mwaka wa 1987 na kanisa la Kiprotestanti pamoja na ubia kati ya Wizara ya Maswala ya Kidini kama kituo cha uelewano wa madhehebu. Kwa wakati huu kituo cha Al Amana kinafanya kazi kimataifa kwa wema wa kawaida kwa niaba ya kujenga madaraja ya uelewano na ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo.

Ratiba za kituo cha Al Amana hutokana na ugunduzi wa maadili ya pamoja kati ya Uislamu na Ukristo. Mipango ya mafunzo ni pamoja na ziara za madhehebu kuhusu maingiliano ya kidini, ratiba za mafunzo ughaibuni, inayofanyika Omani, ratiba za seminari, ratiba ya wasomi wanaohudhuria, uchapishaji, na mkutano wa madhehebu wa kila mwaka.

www.alamanacentre.org