Falsafa ya maingliano

Falsafa ya kiibadhi inatokana na kanuni za uvumilivu wa kidini na kuepukana na ugomvi na vurugu. Maoni mengine ya dini na mitindo mingine ya ufafanuzi wa dini ni lazima uheshimiwe pia.

Sala katika misikiti pote nchini zinafanyika pamoja na Sunni, Shia, bega kwa bega na Ibadhi. Sunni na Shia wakati wote wameishi kwa amani na kupatana bila migogoro yo yote na Ibadhi, ambao kwa wakati huu wote idadi yao iliendelea kuwa kubwa nchini Omani.

Sala za jamaa kwa Mungu hazitambui mabishano ya kitheologia. Kila mtu lazima ajitetee yeye mwenyewe mbele ya mungu, katika kufanya uamuzi kuhusu masuala ya kisheria, Jabir b. Zayd alizingatia yafuatayo kuwa msingi kwa kutoa hukumu za daawa mbele ya jumuia za Waislamu kwa taratibu hii: Qur'an Tukufu, Sunnah, maoni (dhana) ya wazee wa heshima na mwisho uamuzi wa mtu mwenyewe.

Uibadhi una misingi ya wajibu wa kurudia uhalisi wa dini ya Kiislamu na jumuiya na kufuata kamili mwelekeo wa itikadi kama Mtume Mohammed alivyoagiza. Kwa wakati wote Ibadhi wamedumisha uaminifu wao dhabiti kwa Kurani, Sunnah, na kwa Waislamu wenzao, na kila wakati wamekuwa na msimamo wazi kuwaalika watu wengine na kuwapa nafasi ya kuelewa maomi yao, kuwapa muda pia wa kuamua kuhusu misimano yao wenyewe. Wakati wote Ibadhi wameifanya kuwa wazi kwamba hawataweza kupigana na wapinzani wao isipokuwa watashambuliwa kwanza. Umwagaji wa damu kuhusu tofauti za kitheolegia linachukuliwa kama jambo la kuaibisha.

Wakati wote wa historia, wanajumuiya wa madhehebu mbalimbali wameishi Omani: Wayahudi, Wakristo, Wahindi (Baniani) Makalasinga (Sikki) na wengi wengineo. Kutokana na maadili ya stahamala ya kidini kuwepo kwao kulikubaliwa karne zilizopita na hawakubaguliwa dhidi ya ushirikiano wao wa kidini, hata wakati wa utawala wa serikali ya “uimamu” utawala wa kidini.