Maelewano ya pande mbili
Wizara ya fedha (zilizowekwa wakfu) na Mambo kuhusu dini ina wajibu wao kuhusu makundi mbalimbali ya kidini katika jumuia nchini Omani, na makundi mbalimbali haya hukabidhiwa vifaa muhimu kwa kufanya mazoezi ya imani yao.
Makanisa ya Wakristo ya madhehebu mbalimbali yanapatikana Muscat na Salalah, vilevile hekalu za Baniani (Kihindu), Kalasinga pamoja na hekalu za wafuasi wa Budha, zinapatikana maeneo mbalimbali Omani.
Shughuli za usambazaji ujumbe maalum wa kidini zimepigwa marufuku kwa jumuia zote za dini hata zile za Waislamu.
Omani inajitahidi kuonyesha uelewaji wa kweli wa Uislamu, ambayo ni dini ya ukadri, ili kusaidia kupambana na ulokole ambao umeleta usambazaji wa mambo yasiyo sahihi juu ya Uislamu na Waislamu kwa jumla.
Kwa kufanya hivyo Omani hutia moyo kuathiriana kiakili, kiutamanduni kati ya watu, na huweka waziwazi uzoefu wa kutenda mambo kwa kuishi pamoja kwa amani, na stahamala na wana imani kwamba kuna haja za kujenga daraja za uelewano ustahamala na urafiki kati ya watu.